Faida za kufanya usafi na Hasara za kutokufanya usafi ktk Computer Yako.

Kwanza kabisa ninaomba kuanza na utagulizi kama ifuatavyo, tunapo zungumzia usafi ktk Computer tunamaanisha usafi wa aina mbili;

Usafi wa ndani ya Mafaili na Software za Computer (Software and File checkup and maintenance)
Usafi wa vifaa vyote vya ndani na nje ya Computer (Hardware checkup and maintenance)


Ufanyaji usafi ktk Computer yako una faida nyingi sana ikiwemo;

  • Kuongeza urefu wa maisha ya Computer yako
  • Kuongeza umahiri wa Computer yako ktk utendaji kazi
  • Kupunguza gharama za ununuaji vifaa vilivyoharibika kwa kupuuza kufanya usafi
  • Kuepusha Computer kuzimika ghafla kwa kuzidiwa na uchafu au wadudu
  • Kufanya Computer iwe na spidi kama ilivyounuliwa mwanzo



Kutokufanya usafi ktk Computer yako kuna hasara zifuatazo;

  • Inaweza kucrash au kufeli na kuzimika ghafla
  • Spidi ndogo ktk utendaji kazi
  • Kukosa umahiri ktk utendaji kazi, yaani haitakuwa na uwezo wa kufanya kazi kwa muda mrefu na itakuwa inachemka na pengine kuzimika baada ya muda mfupi
  • Gharama kubwa siku ambayo Computer imeharibika sababu itakuwa imeharibu vifaa vingi
  • Utakuwa umeipunguzia urefu wa maisha yake maana haitadumu hata kwa muda wa miaka miwili
N   B  
ufanyaji usafi katika computer mara nyingi katika upande wa hardware hufanywa na ma expart tu ambao wanauwezo wa kuifungua computer vizuri na kufanya usafi bila kusababisha vitu kuharibika

pia ufanyaji wa usafi kwa njia ya software hii inaweza kufanywa na mtu hata asiefahamu hasa maswala ya IT kwa undani kwani mara nyingi hata kuiscan komputre pia ni njia moja wapo ya ufanyaji usafi wa software. hapa tumia antivirus ambazo ni strong alafu ni PRO (usitumie free antivirus sio nzuri sana).


prepared by IBRAHIM MCHUCHURI
Faida za kufanya usafi na Hasara za kutokufanya usafi ktk Computer Yako. Faida za kufanya usafi na Hasara za kutokufanya usafi ktk Computer Yako. Reviewed by Unknown on September 02, 2017 Rating: 5

No comments

Random Posts

3/random/post-list