KWA NINI AKOUNTI YAKO YA GOOGLE ADSENSE UFUNGIWE?

ukiwa na mimi karibu utafaidi mengi kutoka kwangu. sogea hapa na kama kuna rafiki yako anataka awe msasa au aendane na usasa basi lazima awe na ukaribu na maendeleo ya teknolojia kwa ujumla, hivyo nae pia mshauri atambelee hapa, masomo mbalimbali bure yanaendelea.

leo nataka nitoe ushauri na kuwapa elimu juu ya adsense.... tulijadiri sana juu ya adsense kuanzia maana mpka namna ya kujiunga, faida zake na jinsi ya kuziweka kwenye website yako au blogger blog.

kuna maswali mengi nayapokea na malalamiko pia juu ya watumiaji wa google adsense. wengi inafika kipindi wanafungiwa na kama kuna kipato wanakirudisha kwa advertisers wao. kwa kifupi tujadiri kwa nini hali hii inajitokeza hasa kwa bloggers wachanga..... kiukweli inatia huruma sana blogger amepata account ya adsense tena full approval, lakini baadae anafungiwa bila kufahamu ni kwa nini...

kama ulishawahi kutwa na hili nafikili kwenye gmail yako walikutumia ujumbe huu hapa chini...
"Hello,
With our advertising programs, we strive to create an online ecosystem that benefits publishers, advertisers and users. For this reason, we sometimes have to take action against accounts that demonstrate behavior toward users or advertisers that may negatively impact how the ecosystem is perceived. In your case, we have detected invalid activity in your AdSense account and it has been disabled"

ujumbe huo ukipewa jua kuna mambo uliyafanya ambayo yapo kinyume na google adsense privacy policy.. na ndio maana ukafungiwa. sababu kubwa za kufungiwa zipo nyingi lakini zile ambazo wengi zinawaingiza kwenye hali hii ni tatu ambazo nimezieleza hapo chini


SABABU ZA KUFUNGIWA ACCOUNT YAKO YA GOOGLE ADSENSE

  • kubofya matangazo (Ads) wewe mwenyewe. kuna mchezo kwa bloggers wengi kuingia kwenye blog zao na kubofya matangazo ili waongeze kipato, kumbuka google adsense wako makini sana kufuatilia kiundani zaidi ili wakupe malipo mahalali. ni kosa kubwa sana kubofya matangazo wewe mwenyewe kampuni ya google haitoweza kukuvumilia hata kama ulikuwa full approved.
  • adult content. kama umefuatilia kiundani websites na blogs zinazojihusisha na maswala ya adult content hayana matangazo ya google, (kama ukiona matangazo ni company nyingine sio google hao). ni kosa kubwa kuweka adult content kwenye blog yako au website pindi ukikubali masharti ya adsense (google adsense) basi ukikiuka watakufungia iyo account na hautoweza kuunganishwa tena kwa kutumia devices zako.
  • kuingia mara kwa mara. kama wewe ni admini au author wa blog ama website, ukiwa na tabia ya kuingia mara kwa mara kuziangalia post zako ama kwa lengo la kuongeza viewers ili kipato kiongezeke basi itakuwia vigumu kuendelea na google adsense.
NB; ushauri wangu epuka hivyo vitu kuvifanya ili ndoto yako ya kuwa blogger mkubwa zitimie.........


imeandaliwa na IBRAHIM MCHUCHURI
KWA NINI AKOUNTI YAKO YA GOOGLE ADSENSE UFUNGIWE? KWA NINI AKOUNTI  YAKO YA GOOGLE ADSENSE UFUNGIWE? Reviewed by Unknown on June 07, 2017 Rating: 5

1 comment

  1. nimejifuza kitu kikubwa sana kwako ambacho likuwa sikijui ingawa blog yangu ijakamilika bado

    ReplyDelete

Random Posts

3/random/post-list