jinsi ya kulifanya betri la simu yako kufanya kazi kwa muda mrefu bila kuchoka.

habari njema kwa watu wangu mnaopenda kufuatilia, michango yangu na mawazo yangu juu ya teknolojia, na jinsi ya kufaidika nayo.

leo napenda kuwapa kasomo ka faida kwa watumiaji wa simu aina zote yani simu za kawaida na zile zinazokuwa operated by androind OS, yani smartphones.

wengi wetu tunafanya makosa mengi ambayo yanapelekea kutoa malalamiko juu ya ufanisi wa betrii zao (kitunza chaji) kutoishi kwa muda mrefu. sasa leo karibu sana kwenye darasa letu upate kufahamu tips mbalimbali zitakazo kusaidia betri ya simu yako kuishi muda mrefu.

zifuatazo ni mbinu zitakazo kukusaidia kulifanya betrii lako liishi kwa muda mrefu

1. usichaji simu yako kabla ya kufikisha asilimia 15, yani hakikisha unaichaji simu yako baada ya betrii kuisha chaji mpaka kufikia asilimia 15. hapo betri yako itakuwa tayari kuomba msaada.

2. punguza notifications zisizo za lazima kutoka kwenye applications mbalimbali kama vile mitandao ya kijamii na applications zingine ambazo zinatumia umeme mwingi wa simu yako.

3. usiweke chaji simu yako pindi uitumiayo, wengi hutumia simu zao huku wakiweka chaji, lakin ki ukweli wanafanya makosa makubwa sana, kama unataka kutumia simu yako basi usiiweke kwenye chaji. hapo betrii linapungua ufanisi wake wa kazi

4. usslalishe kwenye chaji simu, hili ni kosa kubwa hasa kwa watumiaji wa spartphones, wajenga mazoea ya kuweka chaji pindi wanapopumzika au kulala hasa kipindi cha usiku.

5. punguza mwanga wa simu kwenye simu hii ni kwasababu mwanga unatumia umeme mkubwa sana hivyo lazima uupunguze mwanga ili kulifanya betri lako liwe na maisha marefu.


makala hii imeandaliwa na IBRAHIM MCHUCHURI
jinsi ya kulifanya betri la simu yako kufanya kazi kwa muda mrefu bila kuchoka. jinsi ya kulifanya betri la simu yako kufanya kazi kwa muda mrefu bila kuchoka. Reviewed by Unknown on May 18, 2017 Rating: 5

No comments

Random Posts

3/random/post-list